kiongozi wa kundi hilo Hamad Ally ‘Madii’
amesema kuwa Dogo Janja ameshindwa kuendana na makubaliano halisi
yaliyokuwepo baina yake na uongozi wa kundi hilo ikiwemo kuhudhuria
shuleni kama alivyokuwa akitakiwa kufanya kila siku badala yake
amekuwa akiendekeza starehe na wakati mwingine kufanya mambo ambayo
kwa namna moja ama nyingine yalikuwa yanalichafua kundi hilo.
“Tumemkabidhi
kwa kaka yake mapema leo tukiwa maeneo ya Ubungo tayari kwa safari
ya kurudi kwao na wakati huo tulifanya mawasiliano na baba yake
kumuarifu kuwa Tip Top hatuko na mwanae kwa sasa” alisema Madii
Katika
hatua nyingine Madii amesema kuwa Dogo Janja alilewa sifa na
kujisahau kufanya yale anayotakiwa kufanya ndani nanje ya kundi
kufuatia mafanikio ya muziki aliyoyapata akiwa na Tip Top Connection
kwani hivi karibuni alitega shule na kwenda kujificha nyumbani kwa
TundaMan huku akimuaga Madii kuwa anakwenda shule.
Kuona
hivyo TundaMan aliamaua kumuarifu Madii na mara moja kiongozi huyo wa
kundi aliamua kwenda kumsaka, lakini baada ya dogo Janja kugundua
kuwa Madii anakuja aliamua kukimbia na kwenda kujificha uchochoroni
lakini akiwa huko mafichoni bahati mabaya alikanyaga kuku na siri
yake kujulikana kuwa amejificha hapa na ndipo alipokamatwa na kuamriwa
kufungasha kilicho chake tayari kurejea ‘kileji’.
No comments:
Post a Comment