Saturday, September 1, 2012

WASANII WA BONGO FLEVA NA CLOUDS FM WATOA MSAADA MKOA WA MARA


 



 Baadhi ya Wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a Bongofleva wakiongozwa na baadhi ya Wafanyakazi wa Clouds Media Group wakiwa katika picha ya pamoja jioni ya leo na watoto wanaolelewa  na kituo cha watoto Yatima/waishio katika mazingira sambamba na walezi wao kiitwacho Jipe Moyo Center,kilichopo kata ya Mwisenge,Musoma mjini mkoani Mara.Kampuni ya Clouds Media Group ikishirikiana na wasanii mbalimbali ambao jioni ya leo watatumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,wametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa ajili ya kituo hicho chenye jumla ya watoto 17 waliopo kituoni hapo.

 Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Prof Jay akishiriki kukabidhi sehemu ya msaada kwa niaba ya wasanii wenzake kwa baadhi ya watoto wanaolelewa na kituo hicho,kushoto ni Ofisa Mahusiano wa Clouds Media Group akikabidhi pia sehemu ya msaada uliotolewa na kampuni hiyo kwa walezi wa kituo hicho,kilichopo Musoma Mjini.
 Mratibu Msaidizi wa kituo hicho cha Jipe Moyo Center,Bi.Imelda Odoyo akitoa mkono wa shukurani kwa ujio wao kwa baadhi ya Wasanii  mahiri wa hip hop hapa Bongo Prof. Jay na Fid Q . 
Afisa Mahusiano wa kampuni ya Clouds Media Group,Bwa.Simalenga akizungumza machache kwa niaba ya Kampuni na pia kwa wasanii aliombatana nao,katika suala zima la kukabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vyakula kwa kituo hicho mapema leo jioni,kulia kwake ni Mratibu Msaidizi wa kituo hicho cha Jipe Moyo Center,Bi.Imelda Odoyo na kushoto ni Mratibu wa kazi za kijamii wa kituo hicho,Bwa.Pantaleo Magesa Kuyenga.
Mratibu wa kazi za kijamii wa kituo hicho,Bwa.Pantaleo Magesa Kuyenga akiwakaribisha vyema baadhi ya wafanyakazi wa kampuni ya Clouds Media Group na Wasanii walioambana nao jioni ya leo,akiwemo Prof Jay,Fid Q,Chege,Mwasiti,Bibi Cheke,Omy Dimpo,Bob Junior,Roma,Barnaba na wengineo. 
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,wakiongozwa na mkongwe wa muziki wa Bongofleva,Prof Jay wakitia saini kitabu cha wakati,mara walipowasili kwenye kituo cha Jipe Moyo Center jioni ya leo,wasanii hao watatumbuiza jioni ya leo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ambapo kesho pia watakamua kwenye uwanja wa Kambarage,mjini Sinyanga. 
Mmoja wa wasanii anaekuja kwa kasi katika anga ya bongofleva,Ommy Dimpo a.k.a Pozi kwa Pozi akijitambulisha mbele ya wenyeji,ambapo wageni wote wakiwamo wasanii walijtambulisha.
Mkongwe kwa umri lakini anakamua vilivyo kwenye anga ya bongofleva,Bibi Cheka nae akijitambulisha mbele ya wenyeji.
Sehemu ya misaada kama inavyoonekana mara baada ya kukabidhiwa kwenye kituo hicho.
Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakiwasili kwenye kituo cha kulelea watoto Yatima/waishio katika mazingira magumu kiitwacho Jipe Moyo Center,kilichopo kata ya Mwisenge,Musoma mjini mkoani Mara.Kampuni ya Clouds Media Group ikishirikiana na wasanii mbalimbali ambao jioni ya leo watatumbuiza kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,wametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo chakula kwa ajili ya kituo hicho chenye jumla ya watoto 17 waliopo kituoni hapo.

No comments:

Post a Comment