Profesa Jay akipagawisha.
Mmoja wa ‘Kina Rihanna’ aitwaye Babro, akitetea nafasi yake.
‘Rihanna mwingine’ akiwa kazini.Mmoja wa majaji wa shindano hilo, Baby Madaha (katikati), akiwanadi ‘kina Rihanna’ kwa mashabiki wamchague mmoja aendelee.
Washiriki wanane waliofaulu kuendelea kwenye shindano hilo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Global Publishers Ltd na mmiliki wa Ukumbi wa Dar Live, Eric James Shigongo, akiongea jambo kabla ya zoezi la utoaji tuzo za wasanii wa Hip Hop kuanza.
Msanii wa Hip Hop Bongo, John Mkoloni (kushoto), akikabidhi tuzo kwa mwakilishi wa familia ya Vivian, huku akishuhudiwa na Shigongo.
Mkoloni akikabidhi tuzo nyingine kwa mtoto wa marehemu Complex.
Msanii wa Hip Hop, Joh Makini (kulia), akimkabidhi tuzo mwakilishi wa Father Nelly (kushoto), tukio lililoshuhudiwa na Shigongo.
Profesa Jay (kulia), akikabidhi tuzo kwa familia ya marehemu DJ Kim. Wanaoshuhudia ni mdogo wa DJ Kim na Shigongo.
DJ Choka (kulia), akikabidhi tuzo hiyo kwa mwakilishi wa GWM.
‘Juma Nature’, (kushoto), akikabidhi tuzo kwa mwakilishi wa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, anayeshuhudia ni Shigongo.
Shigongo akiwa amembeba mtoto wa marehemu Complex.
Kundi la ngoma za asili la Mawazo Art Group likitumbuiza mapema ndani ya ukumbi huo.
Mwimbaji wa bendi ya Super Shine Modern Taarab akiwajibika.
Mwimbaji mpya wa Mashauzi Classic Band, Abdul Balki, akinogesha maraha ukumbini.
Jaji mkuu wa shindano la ‘Cheza, Vaa, Imba Kama Rihanna’, Eric Shigongo, akijaribu kumkosoa jambo mmoja wa washiriki.
Moja ya vikundi vya sarakasi kikionyesha uwezo wake.
Sehemu ya umati uliofurika ukumbini hapo.
TAMASHA la Usiku wa Hip Hop kuamkia leo limetikisa vilivyo ndani ya kituo cha maraha cha Dar Live Mbagala-Zakheem jijini Dar es Salaam.
Wasanii waliokuwa kwenye ‘game’ la muziki wa aina hiyo na sasa wametangulia mbele za haki walienziwa kwa kupewa tuzo mbalimbali ambazo zilipokelewa na baadhi ya ndugu zao na marafiki wa karibu.
Wasanii walioenziwa kwa kupewa tuzo ni Mh. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, ambayo ilikabidhiwa na Juma Kassim ‘Juma Nature’ ikimsifu kwa harakati za kuifikisha Hip Hop ilipo leo, nyingine ilikwenda kwa kundi la Kwanza Unit ambayo ilikabidhiwa na Farid Kubanda ‘Fid Q’, ya DJ Kim ilikabidhiwa na Joseph Haule ‘Profesa Jay’, ambapo tuzo ya Bon Love iliyokabidhiwa na Dj Tasi, marehemu Complex tuzo yake ilikabidhiwa na Mkoloni, ambapo tuzo ya GWM ilikabidhiwa na DJ Choka.
Tuzo ya Father Nelly ilikabidhiwa na Joh Makini, ya John Mjema na Steve 2K ilikabidhiwa na G Nako, tuzo ya Saleh Jabir ilikabidhiwa na Big Willy, ya Mr Ebbo ilikabidhiwa na Fanani huku Hard Blasters wakikabidhiwa tena na Juma Nature.
Baada ya Shughuli ya utoaji tuzo, Dar Live ilizizima kwa shoo kali kutoka kwa, Fid Q, Joh Makini, Profesa Jay na wengineo.
Mapema kabla ya zoezi hilo kuanza zilitumbuiza bendi za taarabu za Super Shine na Mashauzi Classic, huku makundi mbalimbali ya ngoma za asili na sarakasi yakitawala ardhi na anga.
Usiku huo pia kulirindima shindano la ‘Cheza, Vaa, Imba Kama Rihanna’ ambapo washiriki wawili waliyaaga mashindano hayo na kubaki washiriki wanane kati ya kumi waliokuwa wameingia kumi bora.
Habari/Picha: Musa Mateja/GPL
No comments:
Post a Comment